Visitors
31 Oktoba 2019
Zimebaki siku 90
EPUKA MSONGAMANO: ZIMEBAKI SIKU 90 KUFIKA MWISHO WA MATUMIZI YA PASIPOTI ZA ZAMANI (MRP). BADILI SASA KUPATA PASIPOTI YA KIELEKTRONIKI. #ePassport, #eVisa, #ePermit, #eBorderManagementSystem
30 Oktoba 2019
Dkt. Makakala aridhishwa na kasi ya ujenzi wa Jengo la Uhamiaji Dodoma.
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna
Makakala na Kamishna wa Utawala na Fedha wa Idara hiyo, amefanya
ukaguzi wa kazi ya ujenzi wa Jengo la Makao Makuu ya Uhamiaji
eneo la NCC, jijini Dodoma. Katika ukaguzi huu Dkt. Makakala ambaye
aliambata na Kamishna wa Uhamiaji Utawala na Fedha Edward Chogero, amesifu
kazi nzuri inayofanywa na wahandisi wa Kampuni ya Kizalendo
ya SUMA JKT ambayo ndiyo iliyopewa zabuni ya ujenzi
wa jengo hilo la ghorofa nane ambalo linalotarajiwa kuwa la
kuvutia jijini humo.
Kazi ya ujenzi wa sehemu ya ardhini ya jengo hilo
imekamilika na kwa sasa maandalizi ya kumwaga zege la jamvi la ghorofa
ya chini yamekamilika na tayari Mshauri Mwelekezi wa Mradi huo ambaye
ni Chuo Kikuu cha Ardhi ametoa idhini ya kumwaga zege
ili kuruhusu hatua zaidi za ujenzi kuendelea.
Ujenzi wa Jengo hilo uinatarajiwa
kukamilika ndani ya muda wa miezi 18, na kwa mujbu wa Meneja
Mradi, Kanali Zablon Mahenge amesema ujenzi unakwenda kwa kasi
na umakini mkubwa na kwamba kazi itakamilika kwa wakati
na ubora wa hali ya juu.
29 Oktoba 2019
27 Oktoba 2019
25 Oktoba 2019
Dkt. MAKAKALA AMPONGEZA KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE KITAIFA 2019
Kamishna
Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Peter Makakala amempongeza Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji Mzee Mkongea Ali kwa kuiwakilisha vyema Idara ya Uhamiaji
katika Mbio za Mwenge Kitaifa Mwaka 2019.
“Nakupongeza
sana kwa kazi nzuri uliofanya katika Taifa letu. Nimefurahi sana kwa uwakilishi
wako uliotukuka, kwa kweli umeibeba vyema bendera ya Uhamiaji, unastahili pongezi
za dhati, pamoja na kwamba uko likizo lakini nimeona nikuite uje nikupongeze”
Alisema Dkt. Makalala
Kwa upande
wake Mkaguzi Msaidizi Mzee Mkongea alimshukuru Kamishna Jenerali, Makamishna na
Viongozi waandamizi wa Idara ya Uhamiaji kwa Miongozo, Ushauri na Maelekezo yao
ya mara kwa mara yaliyomuwezesha kutekeleza majukumu yake ipasavyo wakati wote
wa mbio hizo.
Mzee Mkongea
Ali ambaye ni Afisa Uhamiaji kutoka Ofisi ya Uhamiaji Mjini Magharibi alikuwa Kiongozi
wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kwa Mwaka 2019 ambapo ameifanya kazi hiyo kwa bidii,
uadilifu, utiifu na uzalendo hadi kufikia kilele cha mbio hizo na kuzimwa na Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli
mjini Lindi tarehe 14 Oktoba 2019.
18 Oktoba 2019
UHAMIAJI YASHIRIKI MAONYESHO YA UTALII YA “SWAHILI INTERNATIONAL TOURISM EXPO
Katibu mkuu kiongozi Balozi John kijazi leo amezindua maonyesho ya Utalii ya” SWAHILI INTERNATIONAL TOURISM EXPO katika viwanja vya mlimani city Dar es salaam.
Maonyesho hayo ambayo yameanza leo tarehe18 yatamalizika tarehe 20 mwezi huu yamehusisha taasisi mbalimali ikiwemo idara ya uhamiaji ambapo kama kawaida imeendelea kutoa huduma kwa wageni waalikwa pamoja na wananchi wanaohudhulia maonyesho hayo.
Kwa upande wake mgeni rasmi kwenye maonyesho hayo Balozi Kijazi amesifu maandalizi ya maonyesho hayo na kuwataka wanachi kujitokeza kujua na kujifunza mambo mbalimbali kupitia maonyesho hayo ambayo yanatarajiwa kumalizika Jumapili.
Pia balozi kijazi ameongeza Maonyesho hayo yamesaidia sana kukuza sekta ya utalii ikiwa ni pamoja na kuongeza pato la taifa kupitia sekta ya utalii nchini.
12 Oktoba 2019
Imarisheni doria maeneo yenu” Kamishna Jenerali Dkt. Anna Makakala
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Peter Makakala ametoa agizo hilo alipotembelea ofisi ya Uhamiaji Mkoa Katavi ambapo pamoja na kupata taarifa ya utendaji kazi wa ofisi hiyo na kusikiliza changamoto mbalimbali, aliendelea kusisitiza watumishi wa Idara ya Uhamiaji kufanya kazi kwa kuzingatia sheria na kujiepusha na vitendo vya rushwa.
“Nawataka muimarishe doria katika maeneo yenu hasa katika kipindi hiki tunapokaribia uchaguzi wa serikali za mitaa, maeneo haya yana makambi ya wakimbizi na walowezi. Hakikisheni hawajiingizi kwenye uchaguzi aidha kugombea nafasi za uongozi au kupiga kura.” Aliagiza Dkt. Makakala akiwa Namanyere.
“Mnafanya kazi nzuri sana pamoja na changamoto zilizopo, kila ofisi au kituo nInachopita maneno yangu ni yale yale nakumbusha tu kuwa kila mmoja ajitambue kuwa anatakiwa kufanya kazi kwa mujibu wa sheria, kujiepusha na vitendo vya rushwa pamoja na kuzingatia motto yetu ya Nidhamu, Upendo na Mshikamano miongoni mwenu, Uwajibikaji katika utendaji kazi wenu na kukataa rushwa” alisisitiza Dkt. Makakala.
“Nawataka muimarishe doria katika maeneo yenu hasa katika kipindi hiki tunapokaribia uchaguzi wa serikali za mitaa, maeneo haya yana makambi ya wakimbizi na walowezi. Hakikisheni hawajiingizi kwenye uchaguzi aidha kugombea nafasi za uongozi au kupiga kura.” Aliagiza Dkt. Makakala akiwa Namanyere.
“Mnafanya kazi nzuri sana pamoja na changamoto zilizopo, kila ofisi au kituo nInachopita maneno yangu ni yale yale nakumbusha tu kuwa kila mmoja ajitambue kuwa anatakiwa kufanya kazi kwa mujibu wa sheria, kujiepusha na vitendo vya rushwa pamoja na kuzingatia motto yetu ya Nidhamu, Upendo na Mshikamano miongoni mwenu, Uwajibikaji katika utendaji kazi wenu na kukataa rushwa” alisisitiza Dkt. Makakala.
![]() |
Afisa Uhamiaji Mkoa Katavi, Kamishna Msaidizi wa Uhamiaji Vicent Haule akisoma taarifa ya Utendaji kazi mkoa Katavi mbele ya Kamishna Jenerali Dkt. Makakala. |
![]() |
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Makakala akisaini kitabu cha wageni katika ofisi ya uhamiaji mkoa Katavi alipotembelea mwanzoni mwa wiki hii. |
![]() |
Maafisa Uhamiaji mkoa wa Katavi wakimsikiliza Kamishna Jenerali |
![]() |
Kamishna Jenerali Dkt. Makakala akimsikiliza Afisa Uhamiaji Wilaya ya Nkasi Mrakibu Joseph Bulali wakati alipotembelea ofisi hiyo kuongea na watumishi |
![]() |
Add caption |
![]() |
Kamishna Jenrali akisalimiana na Maafisa wa Ofisi ya Uhamiaji Wilaya ya Nkasi Mkoani Rukwa alipotembelea ofisi hiyo. |
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)