Dar es salaam, Tanzania
Idara ya Uhamiaji Tanzania leo imepokea ugeni kutoka
chuo cha Ulinzi wa Taifa NDC kwa ajili ya ziara ya kupatiwa mafunzo ya namna Idara ya
Uhamiaji inavyofanya shughuli zake katika ulinzi wa Taifa na Maendeleo ya Kiuchumi.
Ziara hiyo ya mafunzo imefanyika katika Ofisi ya
Uhamiaji Kurasini Jijini Dar e salaam ikiongozwa na Brigedia Jenerali Msola na
kupokelewa na Kamishna
wa Uhamiaji Divisheni ya Uraia na Pasipoti Gerald Kihinga ambae alimwakilisha Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Peter Makakala.
Katika mafunzo hayo, mada mbalimbali ziliweza kuwasilishwa na Maafisa kutoka Idara ya uhamiaji hususani Pasipoti, Visa za Kielektroniki, Uraia pamoja na Mifumo inayotumika katika utoaji wa Pasipoti na visa za kieletroniki.
Aidha, Washiriki wa ziara hiyo walipata fursa ya kuuliza maswali na kujibiwa ipasavyo sanjari na kutembelea na kujionea namna mifumo mbalimbali ya Uhamiaji inavyofanya kazi na kuonyesha kufurahishwa na jinsi mifumo hiyo inavyorahisisha utoaji wa huduma za uhamiaji kwa haraka na kwa ufanisi mkubwa.
Kwa upande wao washiriki walimpongeza Kamishna Jenerali wa Uhamiaji kwa mafunzo waliyoyapata na kuongeza kuwa, mafunzo hayo yatawajengea uwezo wa kufanya kazi kwa ufanisi na weledi mkubwa hususani katika kuwahudumia Watanzania, Afrika na Dunia kwa Ujumla.
HABARI NA MATUKIO KATIKA MPICHA
|
Brigedia Jenerali Chelestino Msola (Kushoto) akimkabidhi zawadi kutoka NDC Kamishna wa Uhamiaji Divisheni ya Pasipoti na Uraia Gerald Kihinga anayemwakilisha Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Tanzania |
|
Brigedia Jenerali Chelestino Msola (Kushoto) akimkabidhi zawadi kutoka NDC Kamishna wa Uhamiaji Divisheni ya Pasipoti na Uraia Gerald Kihinga anayemwakilisha Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Tanzania |
|
Brigedia Jenerali Chelestino Msola Mkuu wa Msafara kutoka NDC akisaini kitabu cha Wageni Katika Ofisi ya Uhamiaji Kurasini Dar es salam. |
|
Washiriki wa Mafunzo kutoka NDC wakipewa maelezo mbalimbali kuhusu Huduma zitolewazo na Idara ya Uhamiaji hususani katika Mfumo wa Kidijitali wa Uhamiaji Mtandao walipotembelea moja ya eneo la kutolea huduma hizo |
|
Washiriki kutoka NDC Wakifuatilia kwa makini Mafunzo wanayopewa na Maofisa wa Uhamiaji Tanzania |
|
Kamishna wa Vibali vya Ukaazi na Pasi Mary Palmer Akitolea ufafanuzi kuhusu baadhi ya hoja zilizoulizwa na washiriki kutoka NDC |
|
Baadhi ya washiriki kutoka NDC ambao pia ni kutoka Mataifa mbalimbali wakijitambulisha |
|
Mrakibu wa Uhamiaji Eliud Ikomba akitoa Utangulizi wa Mada iliyotolewa katika Mafunzo ya washiriki kutoka NDC |
|
Mrakibu Msaidizi wa Uhamiaji Azizi Kirondomara Kutoka Kitengo cha Uhusiano Makao Makuu akitoa Mada kwa Washiriki wa Mafunzo kutoka NDC |
|
Baadhi ya Washiriki kutoka Chuo cha Ulinzi NDC wakifuatilia kwa makini mafunzo wanayopewa kuhusa huduma za Idara ya Uhamaiaji Tanzania |
|
Mmoja wa Washiriki Kutoka NDC Akiuliza swali baada ya kupewa mafunzo ya Uhamiaji |
|
Picha ya Pamoja Washiriki wa Mafunzo kutoka NDC Wakiwa na Maofisa wa Uhamiaji Katikati ni Kamishna wa Pasipoti na Uraia Gerald Kihinga (Picha zote na Kitengo cha Uhusiano Makao Makuu) |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni