Kilimanjaro, Tanzania
|
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Dkt Anna Mghwira |
Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Kilimanjaro Kupitia Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda (TRITA) Imeshiriki vyema katika Maadhimisho ya Wiki ya Sheria nchini iliyoambatana na Maonesho kutoka taasisi mbalimbali za Serikali na binafsi ambazo ni wadau wa Mahakama katika kuweka mazingira wezeshi ya Uwekezaji, huku Idara ya Uhamiaji ikiwa ni moja ya wadau muhimu.
Akifungua Maadhimisho hayo Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe Dkt. Anna Mghwira ameitaka Mahakama kutoa haki kwa wote bila kujali uwezo wa kipato kwa wanaokuja kupata huduma za kimahakama katika ofisi husika.
Maadhimisho hayo yalitanguliwa na maandamano yaliyoshirikisha taasisi mbalimbali vikiwemo vyombo vya Ulinzi na Usalama hususani Idara ya Uhamiaji ambapo Mhe. Dkt. Maghwira alipata nafasi ya kutembelea banda la Uhamiaji na kupewa elimu kuhusiana na utolewaji wa pasipoti mpya za kielektoniki na mikakati mbalimbali iliyowekwa na Idara ya Uhamiaji katika kupambana na wimbi la wahamiaji haramu.
Mhe. Mghwira alifurahishwa sana na maelezo yaliyotolewa na Mrakibu Msaidizi wa Uhamiaji Sale Sule ambaye alielezea sheria, kanuni na miongozo inayoendesha Idara.
Aidha Mhe. Maghwira ameitaka Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Kilimanjaro kuongeza nguvu zaidi katika udhibiti wa mipaka na wahamiaji haramu ikiwemo kudhibiti mianya yote inayotumiwa na wahamiaji hao kuingia nchini kinyume na sheria ambapo huweza kuhatarisha usalama wa Taifa.
Maadhimisho hayo yameanza tangu tarehe 31 Januari na yanatariji kuhitimishwa na kilele cha Siku ya Sheria Nchini Tarehe 06 Februari.
Kauli mbiu ya mwaka huu ni “uwekezaji na biashara ni jukumu la mahakama na wadau kuweka mazingira wezeshi ya uwekezaji.
HABARI PICHA NA MATUKIO
|
Mrakibu Msaidizi wa Uhamiaji Sale Sule Aliyeshika Maiki akitoa maelezo ya Banda la Maonesho kwa Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Dkt. Anna Mghwira |
|
Mrakibu Msaidizi wa Uhamiaji Sale Sule Aliyeshika Maiki akimuonesha Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Dkt. Anna Mghwira muonekano wa Pasipoti mpya za Kieleketroniki |
|
Wageni mbalimbali walietembelea Banda la Maonesho la Uhamiaji wakiwa na Shauku kubwa ya kujua taratibu za Upatikanaji wa Pasipoti Mpya ya Kielektroniki |
|
Maafisa Uhamiaji wakiendelea na Utoaji elimu ya Kiuhamiaji |
|
Maandamano ya Maadhimisho ya Ufunguzi wa Wiki ya Sheria Nchini |
|
Mazoezi yakiendelea ili kuoasha mili joto kwa washiriki wa Maadhimisho ya wiki ya Sheria Nchini |
|
(Picha zote na Ofisi ya Uhusiano TRITA) |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni