Dar es salaam, Tanzania
Idara ya Uhamiaji Tanzania imeshiriki Katika Uzinduzi wa Maadhimisho ya Wiki ya sheria nchini yaliyoanza jana katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es salaam.
Maadhimisho hayo yamezinduliwa rasmi mapema leo hii na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe . Paul Makonda ambae amefika na kukagua Banda la maonesho la Idara ya Uhamiaji huku akiridhishwa na huduma zinazotolewa na Idara katika kuwahudumia Watanzania.
Kauli Mbiu ya mwaka huu katika Maonesho haya ni "Uwekezaji na Biashara ni Jukumu la Mahakama na Wadau kuweka mazingira wezeshi ya uwekezaji" ambapo Uhamiaji Tanzania ni moja ya mdau mkubwa na muhimu sana katika uwekezaji hapa nchini.
Idara ya Uhamiaji ni moja kati ya vyombo vya ulinzi na usalama chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ikiwa na jukumu la kutoa vibali vya ukaazi na kudhibiti uingiaji na utokaji wa watu kupitia utekelezaji wa sheria na kanuni zilizopo ili kulinda usalama wa Taifa na kukuza Uchumi wa Taifa.
Maadhimisho hayo yanataraji kuhitimishwa na Siku ya Sheria nchini tarehe 06 Februari 2020 katika viwanja vya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es salaam.
Maadhimisho hayo yanataraji kuhitimishwa na Siku ya Sheria nchini tarehe 06 Februari 2020 katika viwanja vya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es salaam.
Aidha Uhamiaji imedhamiria kuwa taasisi yenye utendaji bora inayotoa huduma za kiuhamiaji zenye kukidhi viwango vya Kitaifa na Kimataifa.
HABARI PICHA NA MATUKIO
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda akipokea maelezo ya Huduma za Kiuhamiaji Kutoka kwa Mrakibu Msaidizi wa Uhamiaji Azizi Kirondomara kutoka Kitengo cha Uhusiano Makao Makuu ya Uhamiaji |
Mkaguzi wa Uhamiaji George Chilundu kutoka Kitengo cha Uhusiano Makao Makuu akifanya Mahojiano na baadhi ya vyombo vya Habari kuelezea huduma zinazotolewa na Uhamiaji Tanzania |
Konstebo wa Uhamiaji Paschal John Kutoka Kitengo cha Uhusiano Makao Makuu akimsikiliza kwa Makini Ofisa wa Polisi wakati anauliza swali juu ya Huduma zitolewazo na Idara ya Uhamiaji Tanzania |
Baadhi ya Wananchi waliotembelea Banda letu kuweza kupata elimu kuhusu Huduma zetu za Kiuhamiaji |
(Picha zote na Kitengo cha Uhusiano Uhamiaji Makao Makuu) |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni