Visitors

IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA UHAMIAJI HABARI BLOGU KARIBU KWENYE BLOG RASMI YA IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA TUNAKULETEA MATUKIO YANAYOTOKEA KILA SIKU KATIKA IDARA YA UHAMIAJI TAFADHALI TUNAOMBA TUFUATILIE PIA KATIKA MITANDAO YETU YA KIJAMII

28 Februari 2020

KAMISHNA JENERALI WA UHAMIAJI AKAGUA UJENZI WA NYUMBA ZA WATUMISHI NA JENGO LA MAKAO MAKUU DODOMA

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna Makakala amefanya ziara ya kutembelea eneo la  Ujenzi wa Mradi wa Nyumba wa Iyumbu Satellite Centre pamoja na NCC panapojengwa Makao Makuu ya Uhamiaji jijini Dodoma leo tarehe 28 Februari 2020.

Idara ya Uhamiaji itegemea kupokea nyumba mpya 40 ikiwa ni sehemu ya pili ya jumla ya nyumba 103 zilizotolewa  na Rais wa awamu ya Tano Mhe. John Joseph Pombe Magufuli kwa ajili ya makazi ya Maafisa, askari na watumishi raia wa Idara hiyo  mwaka 2017.

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna Makakala akisikiliza maelezo ya maendeleo ya umaliziaji ujenzi wa nyumba 40  za Idara hiyo toka kwa Mkurugenzi wa Mauzo, Shirika la Nyumba la Taifa, Ndg. Itandula Gambaladi leo asubuhi, eneo la Iyumbu, jijini Dodoma.


Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna Makakala akisaini Kitabu cha wageni baada ya kuwasili eneo la Karakana ya Ujenzi wa Mradi wa Nyumba wa Iyumbu Satellite Centre jijini Dodoma leo, Idara ya Uhamiaji itegemea kupokea nyumba mpya 40 ikiwa ni sehemu ya pili ya jumla ya nyumba 103 zilizotolewa  na Rais wa awamu ya Tano Mhe. John Joseph Pombe Magufuli kwa ajili ya makazi ya Maafisa, askari na watumishi raia wa Idara hiyo  mwaka 2017.
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna Makakala akikagua Maendeleo ya Ujenzi wa Jengo la Makao Makuu ya Uhamiaji leo asubuhi eneo la NCC, jijini Dodoma.




Hakuna maoni:

Chapisha Maoni