Msemaji
Mkuu wa Idara ya Uhamiaji Tanzania na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano Mrakibu wa
Uhamiaji, Paul John Mselle mapema wiki hii ameendelea na ziara ya utambulisho katika vyombo mbalimbali vya habari.
Ambapo wiki hii ametambulishwa rasmi katika studio
za Azam TV na U FM zilizopo Tabata Jijini Dar es Salaam na kufanya mazungumzo na Uongozi wa Uhai Productions na Watangazaji wa Habari wa Azam TV na U fm Redio.
Tukio
hilo liliratibiwa na aliyekuwa Msemaji Mkuu wa Idara ya Uhamiaji Mrakibu
Mwandamizi, Alhaj Ally Mohamed Mtanda ambaye amehamishiwa Wizara ya Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na kuongozwa Bi. Timzo Kalugira mtangazaji
wa Azam.
|
Mkurugenzi wa Habari Azam Tv Bi. Jane Shirima (katikati) akiwapokea Msemaji Mkuu wa Uhamiaji Tanzani na Aliyekuwa Msemaji wakati wa ziara ya Utambulisho katika studio za Azam Tv mapema wiki hii |
|
Msemaji Mkuu wa Idara ya Uhamiaji Tanzania na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano Mrakibu wa Uhamiaji, Paul John Mselle (Kulia) akifanya mazungumzo na Mtangazaji wa Azam Tv Baraka Mpenja |
|
Bi. Timzo Kalugira Mtangazaji wa Azam Tv wa kwanza (kushoto) akitoa maelezo juu ya utayarishaji na uandaaji wa vipindi unavyofanyika katika studio za Azam Tv
|
|
Baadhi ya Waandishi wa Habari wa Azam Tv Wakiwa katika Majukumu yao ya Kawaida |
|
Ndani ya Studio za 107.3 U fm Dar es salaam |
|
(Picha zote na Kitengo cha Uhusiano Uhamiaji Makao Makuu) |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni