Mtwara,
Tanzania
Idara ya Uhamiaji
Mkoa wa Mtwara imetoa shukrani zake za dhati kwa Kamishna Jenerali wa Uhamiaji
Dkt. Anna Peter Makakala kwa kuongezewa nguvu ya askari wapya 20.
Jumla ya askari wapya
20 waliripoti Mkoani Mtwara mwishoni mwa mwezi Disemba mwaka jana 2019 Mara
baada ya kumaliza mafunzo ya Uhamiaji katika Chuo cha Uongozi cha Jeshi la
Kujenga Taifa JKT-Kimbiji Kilichopo Wilaya ya Kigamboni Jijijini Dar es salaam.
Akitoa Taarifa ya
utendaji kazi ya Mkoa, wakati wa ziara ya Kamishna wa Uhamiaji anayesimamia
Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda (TRITA) Maurice Kitinusa, Afisa Uhamiaji Mkoa wa
Mtwara Kamishna Msaidizi wa Uhamiaji James Mwanjotile alisema mara baada ya
kupata mgao huo aligawa askari hao kwa kila wilaya na vituo vyote vya uhamiaji
mkoani hapo kulingana na mahitaji ya sehemu husika.
“Ujio huu wa askari
wapya afande umesaidia sana kuongeza ufanisi mkubwa katika utendaji wa shughuli
mbalimbali ndani ya Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Mtwara, na kwa muda mfupi tu
tunaona matunda yake ambapo vitendo vingi vya uhalifu wa Kiuhamiaji
vinadhibitiwa ipasavyo, alisema Mwanjotile.
Sanjari na hilo
amevishukuru vyombo vingine vya ulinzi na usalama kwa ushirikiano wanaoutoa
katika utekelezaji wa majukumu mbalimbali ya kiuhamiaji ndani ya mkoa wa mtwara bila kuwasahau wananchi wa mkoa huo ambao
wamekuwa msaada mkubwa wa kutoa taarifa za wahamiaji haramu na kusaidia
kudhibiti vitendo hivyo.
Ikumbukwe kuwa mafanikio yote hayo yanatokana na Juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. John Pombe Magufuli ambae ndie aliyetoa kibali cha Kuajiri Jumla ya Askari wapya 400 waliomaliza mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa JKT, Oparesheni Kikwete na Oparesheni Magufuli Kujitolea na baadae kujiunga na Mafunzo ya Idara ya Uhamiaji, tayari askari hao wametawanywa nchi nzima Tanzania bara na Zanzibar tayari kwa kulitumikia Taifa lao kwa utii, uzalendo weledi na uhodari.
HABARI PICHA NA MATUKIO
|
Kamishna wa Uhamiaji aneyesimamia Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda (TRITA) Maurice Kitinusa akisalimiana na Maofisa askari na Watumishi wa Umma Mkoani Mtwara wakati wa ziara yake hivi karibuni |
|
Kamishna wa Uhamiaji aneyesimamia Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda (TRITA) Maurice Kitinusa akisalimiana na Maofisa askari na Watumishi wa Umma Mkoani Mtwara wakati wa ziara yake hivi karibuni |
|
Kamishna wa Uhamiaji aneyesimamia Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda (TRITA) Maurice Kitinusa akisaini kitabu cha wageni Mkoani Mtwara wakati wa ziara yake hivi karibuni. |
|
Picha na Ofisi ya Uhusiano Uhamiaji Mtwara |
|
Askari wapya wa Idara ya Uhamiaji Tanzania |
|
Askari wapya wa Idara ya Uhamiaji Tanzania |
|
Picha na Maktaba Kutoka Kitengo cha Uhusiano Makao Makuu yan Uhamiaji |
Wadumu Askari wapya ..idumu idara ya uhamiaji
JibuFuta