Iringa, Tanzania
Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Iringa inawashikilia Watuhumiwa (09) kwa makosa ya kiuhamiaji ambapo (07) ni raia wa Ethiopia, (01) raia wa Kenya mwenye
asili ya Somalia na (01) raia wa
Tanzania ambae ni dereva.
Akizungumza na Waandishi wa habari mapema wiki
hii, Afisa Uhamiaji Mkoa wa Iringa - Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhamiaji, Agnes
Michael Luziga alisema, watuhumiwa hao wamekamatwa eneo la Mtera getini na Askari wa Uhamiaji
waliokuwa kwenye doria ya kawaida.
Watuhumiwa hawa wamekamatwa kwa kosa la kuingia nchini
kinyume cha Sheria ya Uhamiaji Sura ya 54 (Immigration Act Cap 54 RE 2016) pamoja
na kanuni zake na watuhumiwa wote wanatarajiwa kufikishwa Mahakamani baada ya
upelelezi wa tuhuma zao kukamilika, aliongeza Kamishna Msaidizi Mwandamizi
Luziga.
Baada ya kuhojiwa na kukaguliwa ilibainika kuwa
watuhumiwa hao walikuwa na pasipoti za
kughushi za Kenya na Ethiopia zikiwa na vibali vya kughushi na wameingia nchini kupitia
njia za panya wakitokea nchini Kenya wakipita kuelekea nchini Afrika Kusini.
Watuhumiwa hao walitumia gari binafsi aina ya Noah
lenye namba za usajili T656 DNP lililokuwa likiendeshwa na dereva raia wa Tanzania
Mosses Apendavyo Mbwambo, Watuhumiwa wengine ni Isse Aliye Abdi, Hussein Hirsi
Ali, Hassan Maalim Adan, Jama Abdulmalik Yuune, Hussein Siyad Ali, Mohhamed Hassan Tikki, Ali Muktar Abdulkadir na
Osman Mohamed Ali.
Aidha, Idara ya Uhamiaji inatoa wito
kwa wamiliki wa vyombo vya usafiri pamoja na madereva kuaacha mara moja
tabia na tamaa za kujishughulisha na biashara haramu ya usafirishaji wa binadamu
kwani ni kinyume na sheria za nchi na hatari kwa usalama wa nchi yetu.
HABARI PICHA NA MATUKIO
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhamiaji Agnes Michael Luziga Afisa Uhamiaji Mkoa wa Iringa |
Watuhumiwa wa Makosa ya Kiuhamiaji waliokamatwa Iringa |
Gari aina ya Noah lililotumika kusafirishia wahamiaji Haramu |
Wahamiaji haramu wakifikishwa katika kituo cha polisi Iringa (Picha zote na Ofisi ya Uhusiano - Uhamiaji Iringa) |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni