Dar es salaam.
Ndege ya Shirika la Ndege Tanzania (Air Tanzania) Iliyotumika kusafirisha mwili wa Marehemu |
Dkt. Makakala akiwa na Maafisa Askari, Watumishi ndugu na jamaa wa Marehemu hapo jana waliuaga mwili wa marehemu katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere(JNIA) tayari kwa kusafirishwa kuelekea Zanzibar kwa ajili ya mazishi ambayo yamefanyika leo kuanzia muda wa saa 10:00 Asubuhi.
Aidha Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Makakala amekabidhi rambirambi ya Tsh. Milioni Moja na elfu hamsini kwa ndugu wa marehemu ikiwa ni ishara ya pole na kuthamini mchango mkubwa wakati wa uhai wake.
Akitoa neno wakati wa kuaga mwili wa marehemu, Dkt. Makakala alisema Taifa limepoteza mtu muhimu na makini sana kwani wakati wa uhai wake na kabla ya kustaafu kazi marehemu alitekeleza majukumu yake ya Idara ya uhamiaji kwa weledi, uzalendo na uhodari wa hali ya juu.
Bwana alitoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe
Ameni.
HABARI PICHA
Mwili wa Marehemu DCI Mstaafu Mwanakhamisi Sheha ukishushwa katika gari maalumu la kubebea maiti tayari kwa kuagwa na kusafirishwa na ndege kuelekea Zanzibar kwa ajili ya mazishi |
Kamishna Jenerali Dkt. Anna Peter Makakala (Kushoto) akikabidhi Rambirambi kwa Wafiwa |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni