Visitors

IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA UHAMIAJI HABARI BLOGU KARIBU KWENYE BLOG RASMI YA IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA TUNAKULETEA MATUKIO YANAYOTOKEA KILA SIKU KATIKA IDARA YA UHAMIAJI TAFADHALI TUNAOMBA TUFUATILIE PIA KATIKA MITANDAO YETU YA KIJAMII

03 Januari 2020

Uhamiaji Saccos yatoa zawadi ya mwaka mpya

Dar es Salaam.

Idara ya Uhamiaji Tanzania kupitia chama chake cha akiba na mikopo Uhamiaji SACCOS mapema wiki hii imetoa zawadi ya mwaka mpya kwenye kituo cha kulelea watoto yatima cha Amani trust kilichopo kigamboni jijini Dar es salaam.

Akizungumza kwa niaba ya Uhamiaji SACCOS mwakilishi wa uhamiaji ambaye pia ni mkuu wa kitengo cha takwimu makao makuu, Naibu Kamishna wa Uhamiaji DCI Asha Mwilima amesema kwa niaba ya kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Peter Makakala wameona watoe zawadi hizo ili kufurahi pamoja na watoto hao ambao wanahitaji msaada hasa katika kipindi hiki cha sherehe za kuuaga mwaka 2019 na kuukaribisha mwaka mpya 2020.

Baadhi ya vifaa vilivyokabidhiwa ni pamoja na Mchele kilo 100 Sembe kilo 50, Sukari kilo 50, Mafuta ya kula lita 50, Mbuzi watatu
Miche ya sabuni 24 pamoja na umeme wa Tsh. laki tatu sawa na units zaidi ya 800.

Akizungumza baada ya kupokea zawadi hizo kwa niaba ya watoto, mlezi wa kituo hicho Bi. Zainab Abdallah amemshukuru kamishna Jenerali kwa msaada huo kupitia Uhamiaji SACCOSS kwani umewasaidia watoto hao kushiriki vyema kipindi cha sikukuu na kupata faraja.

Makabidhiano hayo ya zawadi yalishuhudiwa na Afisa Uhamiaji (W) Kigamboni Mrakibu wa Uhamiaji Christin Mdeme akiambatana na Afisa Uhamiaji (W) Bagamoyo Mrakibu wa Uhamiaji Said Magadula.


HABARI PICHA

 
Maafisa Uhamiaji na Viongozi wa Uhamiaji SACCOS wakiongea na watoto yatima wa kituo cha Amani Trust Kilichopo Kigamboni Jijini Dar es salaam
Afisa Uhamiaji (W) Kigamboni Mrakibu wa Uhamiaji Christin Mdeme akitoa utambulisho wa viongozi aliofuatana nao katika utoaji wa zawadi kwa watoto yatimaBaadhi ya vitu vilivyotolewa msaada kwa watoto yatima

Picha ya pamoja ya viongozi wa Uhamiaji wakiwa na watoto yatima wa kituo cha Amani Trust mara baada ya kuwakabidhi zawadi ya mwaka mpya 
(Picha zote na Ofisi ya Uhusiano Uhamiaji Makao Makuu)


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni