Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Arusha kwa kushirikiana na Mamlaka
ya Vitambulisho vya Taifa wameanzisha Oparesheni maalumu ili kuwezesha wananchi
wengi kupata Vitambulisho vya Taifa kwa wakati kwa kuweka kambi katika Uwanja
wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
Afisa Uhamiaji Mkoa wa Arusha Naibu Kamishna wa
Uhamiaji Abdallah Towo anaongoza timu ya maafisa na askari wa Uhamiaji katika
kutekeleza oparesheni hiyo. Katika oparesheni hii, Idara ya Uhamiaji ina jukumu
la kuthibitisha uraia wa mwombaji wa kitambulisho cha Taifa kabla hajasajiliwa
na kupewa namba na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).
Vitambulisho hivyo pamoja na kuwa utambulisho kwa raia
wa Tanzania na wageni wakazi, pia vinatumika katika usajili wa laini za simu
ambapo awali usajili ulikuwa ufike kikomo tarehe 31 Disemba 2019 lakini Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli
aliongeza siku 20 kuanzia Januari Mosi hadi 20, 2020.
Huduma zikiendelea katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha ambapo mamia ya wakazi wa jiji hilo wameitikia wito kuja kujiandikisha ili kupata vitambulisho vya Taifa. |
Baadhi ya wakazi wa jiji la Arusha waliofika uwanjani kuhudumiwa |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni