Visitors

IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA UHAMIAJI HABARI BLOGU KARIBU KWENYE BLOG RASMI YA IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA TUNAKULETEA MATUKIO YANAYOTOKEA KILA SIKU KATIKA IDARA YA UHAMIAJI TAFADHALI TUNAOMBA TUFUATILIE PIA KATIKA MITANDAO YETU YA KIJAMII

10 Januari 2020

Uhamiaji Iringa yakamata Kundi la Wahamiaji Haramu


Iringa, Tanzania

SACI Agnes Michael Luziga
Afisa Uhamiaji Mkoa wa Iringa
Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Iringa mapema wiki hii inawashikilia watuhumiwa wa makosa ya kiuhamiaji idadi 20 ambapo idadi 19 ni raia wa Kenya wenye asili ya Somalia na raia 01 wa Tanzania.

Akizungumza na vyombo vya habari Afisa Uhamiaji Mkoa wa Iringa Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Uhamiaji SACI Agnes Michael Luziga Alisema Watuhumiwa hawa wameingia nchini kinyume na Sheria ya uhamiaji Sura ya 54 Rejeo la mwaka 2016 (Immigration Act Cap 54 RE 2016)na kanuni zake.

Watuhumiwa hao wamekamatwa mapema wiki hii katika maeneo ya Mtera getini mkoani Iringa na kikosi cha doria cha uhamiaji mkoani hapo mara baada ya kupata taarifa za kiintelejensia kutoka kwa askari wa SUMAJKT Kituo cha getini Mtera.

Wahalifu hao wa uhamiaji haramu waliingia nchini kupitia njia za panya za mpaka wa Namanga mkoa wa Arusha kwa kutumia gari lenye namba za usajili T. 365 DQV aina ya Toyota Alphard na gari namba KCR 537 aina ya Toyota Isisi Piatana lenye usajili wa Kenya wakielekea mkoani Mbeya.

SACI Luziga Amewashukuru askari wa SUMAJKT kwa uzalendo wao mkubwa wa kuilinda nchi yao na kutoa taarifa sehemu husika hadi kufanikisha zoezi la kuwakamata watuhumiwa hao.

Aidha ametoa wito kwa jamii ya Mkoa wa Iringa na Tanzania kwa ujumla kuiga mfano huo wa kuwafichua wahalifu wa aina hiyo kwani Jukumu la  Ulinzi na Usalama wa Taifa na mipaka yake ni la kila mtanzania.

Katika zoezi la kupambana na wahamiaji haramu Idara ya uhamiaji Tanzania inaendelea kutoa elimu kwa umma kwa njia ya Televisheni, Redio, Magazeti, Mikutano ya Hadhara na Mitandao ya kijamii ili kuwaasa wananchi kushiriki kwa kutoa taarifa uhamiaji pindi wanapokutanana na mtu au au kundi la watu ambao wanawatilia mashaka katika maeneo yao ya kazi ili kuwezessha idara kuchunguza na kubaini sababu za ujio wao na shughuli zao hapa nchini.

Wakati huo huo Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Iringa ikiendelea na doria zake imefanikiwa kuwakamata na kuwatia mbaroni watuhumiwa wengine 08 wa makosa ya Kiuhamiaji wakati taratibu za kimahakama zikiendelea.

Mafanikio hayo yote yanatokana na Juhudi kubwa za serikali ya awamu ya tano chini ya kiongozi shupavu Rais na Amiri Jeshi Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli baada ya kuiongezea nguvu idara hii kwa kuajili takribani Askari wapya 400 ambao tayari wameaanza kazi rasmi ya kuitumikia nchi yao na haya ndio matunda tunayoanza kuyaona sasa.

HABARI KATIKA PICHA NA MATUKIO


Watuhumiwa wa uhamiaji haramu wakiwa tayari kuchukiliwa maelezo na maofisa wa idara ya uhamiaji Mkoani Iringa.
Moja ya gari iliyotumika kusafirishia wahamiaji haramu
Gari yenye namba za usajili wa Kenya iliyotumika pia kusafirishia wahamiaji haramu
Wahamiaji haramu wakipakiwa kutoka kituo cha polisi kuelekea Ofisi za Uhamiaji Mkoa wa Iringa kwa ajili ya Mahojiano zaidi
(Picha zote na Kitengo cha Uhusiano Mkoa wa Iringa)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni