Mtwara,
Tanzania
Kamishna wa Uhamiaji anayesimamia Chuo cha
Uhamiaji cha Kikanda (TRITA) Maurice David Kitinusa mapema wikii hii amefanya
ziara ya siku mbili katika Mkoa wa Mtwara na wilaya zake huku akibeba ujumbe wa
Kamishana Jenarali wa Uhamiaji Dkt. Anna Peter Makakala.
Akiongea na Maafisa,
Askari na Watumishi wa Idara ya Uhamiaji Mkoani hapo alisema Kamishna Jenerali
wa Uhamiaji anamshukuru Rais na Amiri Jeshi Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuridhia kuajiri askari wapya 400
waliohitimu mafunzo yao mwezi Disemba mwaka jana 2019 katika Chuo cha Uongozi chaJeshi la Kujenga
Taifa-Kimbiji kilichopo wilaya ya Kigamboni Jijini Dar es salaam, na tayari walishapangiwa vituo mbalimbali vya kazi nchi
nzima na wanachapa kazi ipasavyo.
Mbali na idadi hiyo
kuongezeka bado tuna uhitaji mkubwa wa watumishi ndani ya idara yetu kwani
malengo ni kufikia askari elfu ishirini (20,000).
Hivyo kutokana na
upungufu huo kamishina Jenerali amewataka watumishi wote waliopo kufanya kazi
kwa bidii, weledi, uzalendo utii na uhodari wa hali ya juu wakati changamoto
hiyo ikiendelea kutatuliwa kama ilivyooneshwa nia na Rais Magufuli.
Aidha ameendelea
kusisitiza Utoaji wa huduma bora na ukusanyaji wa maduhuli ya serikali na
kuhakikisha Idara inatimiza malengo yake ya kukusanya maduhuli kwa ajili ya
maendeleo na uchumi wa Taifa.
Katika ujumbe huo
kamishna Jenerali wa Uhamiaji amewaasa Maafisa, Askari, na Watumishi wote ndani
ya Idara ya Uhamiaji kujiepusha na rushwa na kufanya kazi kwa weledi zaidi.
Kutokana na tatizo la
wahamiaji haramu ndani ya nchi, Kamishina Jenerali amewataka askari na
watumishi wengine wa Idara ya Uhamiaji kuhakikisha wanakabiliana na tatizo hilo
kwa kuendesha Oparesheni maalumu, akifafanua ujumbe huo Kamishna Maurice Kitunusa
ametoa agizo la kufanyika kwa Oparesheni maalumu ya kuwabaini wahamiaji haramu
waliopo ndani ya nchi na kuwachukulia hatua ikiwa ni pamoja na kuwafikisha
mahakamani.
Pia amesisitiza
kutumia vyombo vya habari nchini yaani T.V, redio, magazeti na mitandao ya
kijamii ili kuuhabarisha umma juu ya kinachoendelea katika oparesheni hiyo na
Kuendelea kutoa elimu kwa umma juu ya madhara ya kuruhusu wahamiaji haramu
katika nchi yetu ambapo ni hatari kwa usalama wa Taifa na Dunia kwa ujumla.
Kamishna Kitunusa aliwasili Mkoani Mtwara akitokea Mkoa wa Lindi na Kupokelewa na Mwenyeji wake Afisa Uhamiaji Mkoa wa Mtwara Kamishna Msaidizi James A. Mwanjotile huku akikagua maendeleo ya ujenzi wa Jengo Jipya la Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Mtwara na baadae kutembelea daraja la umoja linalotenganisha Wilaya ya Nanyumbu na Nchi ya Msumbiji.
HABARI PICHA NA MATUKIO
Kamishna wa Uhamiaji anayesimamia Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda (TRITA) Maurice David Kitinusa akiwasilikatika Ofisi za Uhamiaji Mkoani Mtwara |
Kamishna wa Uhamiaji anayesimamia Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda (TRITA) Maurice David Kitinusa (katikati) akiwa katika ofisi ya Afisa Uhamiaji Mkoa wa Mtwara tayari kwa kupokea taarifa ya Uhamiaji Mkoa kutoka kwa Mwenyeji wake Afisa Uhamiaji Mkoa wa Mtwara Kamishna Msaidizi James A. Mwanjotile |
Kamishna wa Uhamiaji anayesimamia Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda (TRITA) Maurice David Kitinusa akisalimiana na Maofisa na Askari wa Ofisi ya Uhamiji Wilaya ya Masasi |
Pichani Ujenzi wa Jengo Jipya la Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Mtwara ukiendelea. |
Kamishna Kitinusa alipotembelea daraja la umoja linalotenganisha Wilaya ya Nanyumbu na Nchi ya Msumbiji. |
Daraja la umoja linalotenganisha Nchi ya Tanzania na Msumbiji katika Wilaya ya Nanyumbu. |
Picha zote na Ofisi ya Uhusiano Uhamiaji Mkoa wa Mtwara |
Nzuri iyo
JibuFuta