 |
Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud Sururu akizungumza na Watumishi wa Uhamiaji katika Ofisi ya Uhamiaji Kaskazini Pemba.
|
Kamishna
wa Uhamiaji Zanzibar Johari M. Sururu amewataka Askari na Maafisa wa Idara ya Uhamiaji kufanya kazi kwa weledi na kujituma ili
kuweza kutekeleza vyema majukumu yao ya msingi ya kusimamia na kudhibiti
Uingiaji, Ukaaji na Utokaji wa Watu Nchini wakati wa majumuisho ya kuhitimisha ziara yake katika Mikoa ya Kusini na
Kaskazini Pemba iliyoanza tarehe 18 – 21 Disemba, 2017.
Akizungumza na Watumishi katika ziara hiyo Kamishna Sururu alisema,“Ili kuimarisha utendaji wetu ni
vyema kuacha kufanya kazi kwa mazowea na muda wote, tutoe huduma za Uhamiaji
bila ya Upendeleo, Unyanyasaji au Ucheleshwaji usio wa lazima. Tutumie lugha
nzuri na tutekeleze kwa vitendo dhana ya kumjali Mteja katika misingi ya sheria, kanuni na maadili ya utumishi wa umma''
.
Aidha, katika ziara hiyo, Kamishna Sururu alifika katika vipenyo na Bandari Bubu zinazotumiwa na wakaazi
wa maeneo hayo, kwa shughuli mbali mbali zikiwemo za uvuvi na biashara haramu ya kuingiza Wahamaiji haramu nchini wakitokea Nchi mbali mbali tunazopakana nazo kwa upande wa bahari ya Hindi. Kisiwa cha Pemba kinasemekana kuwa na
Bandari bubu zaidi ya mia tatu (300) ambazo zinatumiwa na wahalifu hao kusafirisha Wahamiaji na magendo, Wilaya za Micheweni, Wete na Mkoani ndizo zizoathiriwa zaidi na vitendo hivyo dhalimu.
Kadhalika, Kamishna Sururu alimtembelea Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Bwana Omari Khamis Othman, Viongozi wa Mamlaka ya Bandari Pemba na aliongea na baadhi ya wananchi ambapo alisikiliza kero zao na kuahidi kuzipatia ufumbuzi.

Kamishna
wa Uhamiaji Zanzibar, Johari M. Sururu akipokea salamu kutoka kwa Askari wa
Jeshi la Uhamiaji Mkoa wa Kaskazini Pemba, wakati akiwasili Ofisi hapo kwa
ziara ya kikazi Mkoani humo tarehe 20 - 21 Disemba, 2017. Kushoto ni Afisa
Uhamiaji Mkoa wa Kaskazini Pemba, Naibu Kamishna wa Uhamiaji Asumsio Achacha.
Mkaguzi
Msaidizi wa Uhamiaji, Said M. Samaki akichangia hoja katika kikao cha pamoja na
Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar na Wafanyakazi wote wa Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Sheha
wa Shehia ya Shumba Mjini, Bi. Rahma Mohamed Shaame (katikati) akimueleza
Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari M. Sururu (kushoto kwake), kuhusu
matumizi ya Bandari bubu Shumba Mjini inayotumiwa na wakaazi wengi wa Wilaya ya
Micheweni kufanya safari zao za kibiashara kwenda Visiwa vya Mombasa Kenya.
Sheha wa Shehia ya Kiuyu Mbuyuni, Bw. Ali Hamad
Sharifu (wa pili kulia) akimueleza Kamishna wa Uhamiaji (Zanzibar), Johari M.
Sururu (kushoto kwake), jinsi wanavyoshirikiana na watendaji wa Idara ya
Uhamiaji kwa kutoa taarifa zinazosaidia kuwadhibiti baadhi ya Watu wasio
waaminifu wanaojaribu kuingiza wageni bila ya kufuata Sheria na Taratibu za
Idara ya Uhamiaji Nchini.
Tumbe ni
mojawapo ya Bandari Bubu zilizopo ndani ya Wilaya ya Micheweni, Mkoa wa
Kaskazini Pemba.