Visitors
31 Januari 2020
Oparesheni Maalumu ya Uhamiaji Mkoa wa Mara yazaa Matunda
Mara,
Tanzania
Idara ya Uhamiaji
Mkoa wa Mara inaendesha Oparesheni Maalum ya kudhibiti Wahamiaji haramu kwa
kukagua viwanda, mashule, taasisi za dini, migodi, hoteli na nyumba za kulala
wageni na kufanikiwa kukamata Jumla ya wageni 109, ambao wamekutwa na makosa
mbalimbali ya kiuhamiaji kama vile kufanya kazi bila vibali, kuingia nchini
kinyume cha taratibu na wengine kuzidisha muda wa ruhusa zao walizopewa kwenye vituo vya kuingia nchini (entry point).
![]() |
Afisa Uhamiaji Mkoa wa Mara Naibu Kamishna Albert Rwelamila |
Akizungumza na Waandishi wa Habari Ofisini kwake Afisa
Uhamiaji Mkoa wa Mara Naibu Kamishna (DCI) Albert Rwelamila alisema lengo la
Operesheni hiyo ni utekelezaji wa
mkakati wa Idara ya Uhamiaji wa kudhibiti Uhamiaji usio zingatia sheria
ambao ulizinduliwa mwezi septemba mwaka 2019.
Hadi kufikia leo Uhamiaji Mkoa wa
Mara imekamata wahamiaji hao haramu wakiwemo wenye utata wa uraia, ambao wanaotoka katika nchi
mbalimbali za Uganda, Kenya, Rwanda, Armenia, Urusi, Korea, Australia, Afrika Kusini, Nigeria, Uingereza Ethiopia, China, Congo, Senegal, India, na Indonesia.
Aidha Naibu Kamishna Rwelamila aliongeza kuwa wamekamata pia raia wengine wa kigeni ambao
wamejiandikisha katika daftari la wapiga kura na wengine vitambulisho vya
taifa, ambapo idara imefanikiwa kuzuia kwa muda nyaraka hizo kwa uchunguzi zaidi zikiwa idadi nyaraka 24.
Jumla ya Kesi saba
zimefikishwa katika mahakama ya wilaya ya Musoma, kwa makosa ya kuingia na
kuishi nchini kinyume cha sheria ya Uhamiaj ya Sura ya 54 Rejeo la Mwaka 2016 na Kanuni zake, ambapo watuhumiwa watano walikutwa na hatia na kuhukumiwa kwenda jela miaka mitatu
au kulipa faini ya Tsh 500,000/=, watatu
wamelipa faini na kuondoshwa nchini, watuhumiwa wawili wanatumikia kifungo
pamoja na watuhumiwa wengine wawili kesi zao bado zinendelea mahakamani.
“Operesheni hii
bado inaendelea na tunawataadharisha wageni kufuata uraratibu wa kuingia na
kuishi nchini pamoja na kutii sheria bila shuruti” aliongeza Naibu Kamishna Rwelamira
Sanjari na hilo
Afisa Uhamiaji Mkoa wa Mara ametoa wito kwa Wageni wanapoingia nchini,
wanatakiwa kuwa na Pasipoti halisi ya kusafiria kutoka katika nchi yake au hati yoyote ya kusafiria, apate ruhusa, kulingana na dhumuni la safari yake na pia apite katika kituo rasmi cha kuingilia nchini.
Ikiwa mgeni anataka
kuja kufanya kazi hapa nchini anatakiwa kuomba kibali cha kazi
kutoka katika Wizara ya Kazi Ajira na walemavu na baadae kuomba kibali cha
ukaazi ambacho kinatolewa na Idara ya Uhamiaji.
Operesheni hiyo, maalumu ilipewa baraka na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Peter Makakala, katika Mkoa wa Mara ikiwa na lengo la kuthibiti wahamiaji haramu ambao wanaweza kuhatarisha Usalama wa Taifa letu na inaendelea kufanyika kwa ufanisi mkubwa baada ya kuongezewa nguvu ya Askari wapya walioajiriwa hivi karibuni na kusambazwa katika Wilaya zote za Mkoa wa Mara ambazo ni Bunda, Musoma, Tarime, Serengeti, Rorya na Butiama.
HABARI PICHA NA MATUKIO
![]() |
Afisa Uhamiaji Mkoa wa Mara Naibu Kamishna Albert Rwelamila (kulia) akionesha baadhi ya Vyeti vya kuzaliwa vilivyopatikana kinyume na sheria. |
![]() |
(Picha zote na Ofisi ya Uhusiano Uhamiaji Mkoa wa Mara) |
30 Januari 2020
UHAMIAJI Iringa Kinara wa Kukamata Wahamiaji Haramu
Iringa, Tanzania

Akiongea na waandishi wa habari Ofisini kwake, Afisa Uhamiaji Mkoa wa Iringa Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhamiaji (SACI) Agnes Michael Luziga alisema, watuhumiwa wote wamekamatwa eneo la Igumbilo lililopo karibia na Kituo Kikuu cha mabasi Iringa na Kikosi Maalumu cha doria cha Askari wa Uhamiaji wakati wakitekeleza majukumu yao ya kila siku.
Baada ya kuhojiwa imebainika kuwa watuhumiwa hao walikuwa wametelekezwa na wenyeji wao na walikuwa wanapita katika njia za panya maeneo ya nje kidogo ya Manispaa ya Iringa na walikuwa wanaelekea nchini Afrika ya Kusini kupitia Malawi, aliongeza Kamishna Msaidizi Mwandamizi Luziga.
Watuhumiwa wote wanatarajiwa kufikishwa Mahakamani kwa kosa la kuingia nchini kinyume cha Sheria ya Uhamiaji Sura 54, Rejeo la Mwaka 2016 pamoja na Kanuni zake.
Aidha, Idara ya Uhamiaji inatoa wito kwa watu wasiowadilifu na wanaojihushisha na biashara haramu ya usafirishaji wa binadamu kuacha mara moja.
Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Iringa inaendelea kufanya doria na oparesheni mbalimbali kwa lengo la kuwabaini na kuwakamata watuhumiwa wote wanaoishi nchini kinyume cha Sheria na kuwafikisha Mahakamani na hatimaye kuwaondosha nchini.
Ikumbukwe kuwa ndani ya mwezi mmoja tu wa Januari 2020 Uhamiaji Mkoa wa Iringa imefanikiwa kukamata wahamiaji haramu zaidi ya mara tatu mfululizo.
HABARI PICHA NA MATUKIO
![]() |
Afisa Uhamiaji Mkoa wa Iringa Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhamiaji (SACI) Agnes Michael Luziga |
![]() |
Afisa Uhamiaji Mkoa wa Iringa Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhamiaji (SACI) Agnes Michael Luziga (Kulia) akiwa na Afisa Uhamiaji Msaidizi Mkoa Kamishna Msaidizi (ACI) Peter Joseph Kimario |
![]() |
Watuhumiwa waliokamatwa |
![]() |
(Picha zote na Ofisi ya Uhusiano Mkoa wa Iringa) |
28 Januari 2020
UHAMIAJI Mtwara Yamshukuru CGI Kwa Kuongezewa Askari Wapya 20
Mtwara,
Tanzania
Idara ya Uhamiaji
Mkoa wa Mtwara imetoa shukrani zake za dhati kwa Kamishna Jenerali wa Uhamiaji
Dkt. Anna Peter Makakala kwa kuongezewa nguvu ya askari wapya 20.
Jumla ya askari wapya
20 waliripoti Mkoani Mtwara mwishoni mwa mwezi Disemba mwaka jana 2019 Mara
baada ya kumaliza mafunzo ya Uhamiaji katika Chuo cha Uongozi cha Jeshi la
Kujenga Taifa JKT-Kimbiji Kilichopo Wilaya ya Kigamboni Jijijini Dar es salaam.
Akitoa Taarifa ya
utendaji kazi ya Mkoa, wakati wa ziara ya Kamishna wa Uhamiaji anayesimamia
Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda (TRITA) Maurice Kitinusa, Afisa Uhamiaji Mkoa wa
Mtwara Kamishna Msaidizi wa Uhamiaji James Mwanjotile alisema mara baada ya
kupata mgao huo aligawa askari hao kwa kila wilaya na vituo vyote vya uhamiaji
mkoani hapo kulingana na mahitaji ya sehemu husika.
“Ujio huu wa askari
wapya afande umesaidia sana kuongeza ufanisi mkubwa katika utendaji wa shughuli
mbalimbali ndani ya Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Mtwara, na kwa muda mfupi tu
tunaona matunda yake ambapo vitendo vingi vya uhalifu wa Kiuhamiaji
vinadhibitiwa ipasavyo, alisema Mwanjotile.
Sanjari na hilo
amevishukuru vyombo vingine vya ulinzi na usalama kwa ushirikiano wanaoutoa
katika utekelezaji wa majukumu mbalimbali ya kiuhamiaji ndani ya mkoa wa mtwara bila kuwasahau wananchi wa mkoa huo ambao
wamekuwa msaada mkubwa wa kutoa taarifa za wahamiaji haramu na kusaidia
kudhibiti vitendo hivyo.
Ikumbukwe kuwa mafanikio yote hayo yanatokana na Juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. John Pombe Magufuli ambae ndie aliyetoa kibali cha Kuajiri Jumla ya Askari wapya 400 waliomaliza mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa JKT, Oparesheni Kikwete na Oparesheni Magufuli Kujitolea na baadae kujiunga na Mafunzo ya Idara ya Uhamiaji, tayari askari hao wametawanywa nchi nzima Tanzania bara na Zanzibar tayari kwa kulitumikia Taifa lao kwa utii, uzalendo weledi na uhodari.
HABARI PICHA NA MATUKIO
![]() |
Kamishna wa Uhamiaji aneyesimamia Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda (TRITA) Maurice Kitinusa akisalimiana na Maofisa askari na Watumishi wa Umma Mkoani Mtwara wakati wa ziara yake hivi karibuni |
![]() |
Kamishna wa Uhamiaji aneyesimamia Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda (TRITA) Maurice Kitinusa akisalimiana na Maofisa askari na Watumishi wa Umma Mkoani Mtwara wakati wa ziara yake hivi karibuni |
![]() |
Kamishna wa Uhamiaji aneyesimamia Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda (TRITA) Maurice Kitinusa akisaini kitabu cha wageni Mkoani Mtwara wakati wa ziara yake hivi karibuni. |
![]() |
Picha na Ofisi ya Uhusiano Uhamiaji Mtwara |
Askari wapya wa Idara ya Uhamiaji Tanzania |
Askari wapya wa Idara ya Uhamiaji Tanzania |
Picha na Maktaba Kutoka Kitengo cha Uhusiano Makao Makuu yan Uhamiaji |
27 Januari 2020
Kamishna Kitinusa Apeleka Ujumbe wa CGI Mtwara na Kumshukuru Rais Magufuli kwa Kuajiri Askari wapya 400.
Mtwara,
Tanzania

Akiongea na Maafisa,
Askari na Watumishi wa Idara ya Uhamiaji Mkoani hapo alisema Kamishna Jenerali
wa Uhamiaji anamshukuru Rais na Amiri Jeshi Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuridhia kuajiri askari wapya 400
waliohitimu mafunzo yao mwezi Disemba mwaka jana 2019 katika Chuo cha Uongozi chaJeshi la Kujenga
Taifa-Kimbiji kilichopo wilaya ya Kigamboni Jijini Dar es salaam, na tayari walishapangiwa vituo mbalimbali vya kazi nchi
nzima na wanachapa kazi ipasavyo.
Mbali na idadi hiyo
kuongezeka bado tuna uhitaji mkubwa wa watumishi ndani ya idara yetu kwani
malengo ni kufikia askari elfu ishirini (20,000).
Hivyo kutokana na
upungufu huo kamishina Jenerali amewataka watumishi wote waliopo kufanya kazi
kwa bidii, weledi, uzalendo utii na uhodari wa hali ya juu wakati changamoto
hiyo ikiendelea kutatuliwa kama ilivyooneshwa nia na Rais Magufuli.
Aidha ameendelea
kusisitiza Utoaji wa huduma bora na ukusanyaji wa maduhuli ya serikali na
kuhakikisha Idara inatimiza malengo yake ya kukusanya maduhuli kwa ajili ya
maendeleo na uchumi wa Taifa.
Katika ujumbe huo
kamishna Jenerali wa Uhamiaji amewaasa Maafisa, Askari, na Watumishi wote ndani
ya Idara ya Uhamiaji kujiepusha na rushwa na kufanya kazi kwa weledi zaidi.
Kutokana na tatizo la
wahamiaji haramu ndani ya nchi, Kamishina Jenerali amewataka askari na
watumishi wengine wa Idara ya Uhamiaji kuhakikisha wanakabiliana na tatizo hilo
kwa kuendesha Oparesheni maalumu, akifafanua ujumbe huo Kamishna Maurice Kitunusa
ametoa agizo la kufanyika kwa Oparesheni maalumu ya kuwabaini wahamiaji haramu
waliopo ndani ya nchi na kuwachukulia hatua ikiwa ni pamoja na kuwafikisha
mahakamani.
Pia amesisitiza
kutumia vyombo vya habari nchini yaani T.V, redio, magazeti na mitandao ya
kijamii ili kuuhabarisha umma juu ya kinachoendelea katika oparesheni hiyo na
Kuendelea kutoa elimu kwa umma juu ya madhara ya kuruhusu wahamiaji haramu
katika nchi yetu ambapo ni hatari kwa usalama wa Taifa na Dunia kwa ujumla.
Kamishna Kitunusa aliwasili Mkoani Mtwara akitokea Mkoa wa Lindi na Kupokelewa na Mwenyeji wake Afisa Uhamiaji Mkoa wa Mtwara Kamishna Msaidizi James A. Mwanjotile huku akikagua maendeleo ya ujenzi wa Jengo Jipya la Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Mtwara na baadae kutembelea daraja la umoja linalotenganisha Wilaya ya Nanyumbu na Nchi ya Msumbiji.
HABARI PICHA NA MATUKIO
![]() |
Kamishna wa Uhamiaji anayesimamia Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda (TRITA) Maurice David Kitinusa akiwasilikatika Ofisi za Uhamiaji Mkoani Mtwara |
![]() |
Kamishna wa Uhamiaji anayesimamia Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda (TRITA) Maurice David Kitinusa (katikati) akiwa katika ofisi ya Afisa Uhamiaji Mkoa wa Mtwara tayari kwa kupokea taarifa ya Uhamiaji Mkoa kutoka kwa Mwenyeji wake Afisa Uhamiaji Mkoa wa Mtwara Kamishna Msaidizi James A. Mwanjotile |
![]() |
Kamishna wa Uhamiaji anayesimamia Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda (TRITA) Maurice David Kitinusa akisalimiana na Maofisa na Askari wa Ofisi ya Uhamiji Wilaya ya Masasi |
![]() |
Pichani Ujenzi wa Jengo Jipya la Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Mtwara ukiendelea. |

![]() |
Kamishna Kitinusa alipotembelea daraja la umoja linalotenganisha Wilaya ya Nanyumbu na Nchi ya Msumbiji. |
![]() |
Daraja la umoja linalotenganisha Nchi ya Tanzania na Msumbiji katika Wilaya ya Nanyumbu. |
![]() |
Picha zote na Ofisi ya Uhusiano Uhamiaji Mkoa wa Mtwara |
24 Januari 2020
22 Januari 2020
Uhamiaji Iringa yakamata tena Wahamiaji Haramu
Iringa, Tanzania

Akizungumza na Waandishi wa habari mapema wiki
hii, Afisa Uhamiaji Mkoa wa Iringa - Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhamiaji, Agnes
Michael Luziga alisema, watuhumiwa hao wamekamatwa eneo la Mtera getini na Askari wa Uhamiaji
waliokuwa kwenye doria ya kawaida.
Watuhumiwa hawa wamekamatwa kwa kosa la kuingia nchini
kinyume cha Sheria ya Uhamiaji Sura ya 54 (Immigration Act Cap 54 RE 2016) pamoja
na kanuni zake na watuhumiwa wote wanatarajiwa kufikishwa Mahakamani baada ya
upelelezi wa tuhuma zao kukamilika, aliongeza Kamishna Msaidizi Mwandamizi
Luziga.
Baada ya kuhojiwa na kukaguliwa ilibainika kuwa
watuhumiwa hao walikuwa na pasipoti za
kughushi za Kenya na Ethiopia zikiwa na vibali vya kughushi na wameingia nchini kupitia
njia za panya wakitokea nchini Kenya wakipita kuelekea nchini Afrika Kusini.
Watuhumiwa hao walitumia gari binafsi aina ya Noah
lenye namba za usajili T656 DNP lililokuwa likiendeshwa na dereva raia wa Tanzania
Mosses Apendavyo Mbwambo, Watuhumiwa wengine ni Isse Aliye Abdi, Hussein Hirsi
Ali, Hassan Maalim Adan, Jama Abdulmalik Yuune, Hussein Siyad Ali, Mohhamed Hassan Tikki, Ali Muktar Abdulkadir na
Osman Mohamed Ali.
Aidha, Idara ya Uhamiaji inatoa wito
kwa wamiliki wa vyombo vya usafiri pamoja na madereva kuaacha mara moja
tabia na tamaa za kujishughulisha na biashara haramu ya usafirishaji wa binadamu
kwani ni kinyume na sheria za nchi na hatari kwa usalama wa nchi yetu.
HABARI PICHA NA MATUKIO
![]() |
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhamiaji Agnes Michael Luziga Afisa Uhamiaji Mkoa wa Iringa |
![]() |
Watuhumiwa wa Makosa ya Kiuhamiaji waliokamatwa Iringa |
![]() |
Gari aina ya Noah lililotumika kusafirishia wahamiaji Haramu |
![]() |
Wahamiaji haramu wakifikishwa katika kituo cha polisi Iringa (Picha zote na Ofisi ya Uhusiano - Uhamiaji Iringa) |
20 Januari 2020
IOM na Uhamiaji Tanzania zashirikiana kuendesha Mafunzo Mpakani mwa Tanzania na Kenya.
IOM Tanzania
inatekeleza miradi mingi hapa Afrika hususani nchini Tanzania na sasa wakishirikiana
na Idara ya Uhamiaji Tanzania wanatekeleza mradi huu wa kampeni ya utoaji elimu
kwa umma kuhusu masuala ya kiuhamiaji mipakani ikiwa na lengo kuu la kutatua
changamoto wanazokutana nazo wananchi waishio mipakani na kuwajengea uwezo ili
kuwa na uhusiano mzuri wa kuwezesha ulinzi na usalama na hatimae kupambana na
uhalifu unaotokea mipakani.
Akifungua rasmi
mafunzo hayo ya kuwajengea uwezo wawakilishi wa wananchi, Mkuu wa Wilaya ya
Mkinga Yona Maki amelishukuru Shirika la Umoja wa Mataifa la Wahamaji (IOM)
na Idara ya Uhamiaji Tanzania kwa kuwaletea fursa hiyo ya mafunzo kwa wananchi
wake ili kusaidia kupunguza vitendo vya kihalifu vinavyotokea katika mpaka wa
Kenya na Tanzania.
Vitendo hivyo vya
kihalifu vinasababishwa na kutokuwa na elimu sahihi ya jinsi ya kuishi mipakani
na namna ya kuwabaini wahamiaji haramu ambao wanaweza kuhatarisha usalama wa
Taifa na wananchi kwa ujumla.
“Tunapoishi mipakani
kuna shughuli nyingi zinafanyika, wengine mnasafirisha magendo, wengine
mnasafirisha wahamiaji haramu ili kujipatia fedha, lakini leo wamekuja
wataalamu wetu na wanatufundisha madhara ya kufanya shughuli haramu kama hizo
ni kosa la jinai hivyo yazingatieni sana mafunzo haya kwa faida ya kizazi cha
sasa na baadae” alisema Bwana Maki.
Aidha ameendelea
kuishukuru serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa
kuiwezesha Idara ya Uhamiaji kuendelea kutekeleza majukumu yake ipasavyo ikiwa
ni pamoja na utoaji elimu kwa umma na wanavyoshirikiana kwa karibu na shirika
hili la IOM jambo ambalo limesaidia sana kupungua kwa vitendo vya kihalifu
katika mipaka ya nchi yetu hasa katika Mkoa wa Tanga.
“IOM na Idara ya
Uhamiaji Wamekuwa ni wadau wetu wakubwa sana kwani wameendelea kutuletea
mafunzo kama haya kwa zaidi ya mara tatu sasa wanafika katika maeneo yetu ya
Wilaya ya Mkinga na kutupa elimu hii muhimu sana” alisema.
Kwa upande wake Afisa
Uhusiano kutoka Idara ya Uhamiaji Makao Makuu Mrakibu Msaidizi, Azizi
Kirondomara akitambulisha mada zilizofundishwa alisema washiriki wamefundishwa
aina za uhalifu unaovuka mipaka, usafirishaji haramu wa binadamu, usafirishaji
kimagendo, ugaidi usafirishaji silaha haramu, uingizaji bidhaa feki, utakatishaji
fedha, madawa ya kulevya, uhalifu wa kimtandao, na taratibu za kuingia nchini.
Aidha amebainisha
madhara yanayoweza kutokea endapo wahamiaji haramu watapenya na kuingia hapa
nchini, ambapo hupelekea kuhatarisha usalama wa Taifa, kuongeza mzigo serikali
katika utoaji wa huduma za jamii, kuongezeka kwa vitendo vya kihalifu, kupungua
kwa nafasi za ajira, kuchochea migogoro baina ya wafugaji na wakullima na pia
wahamiaji holela kushiriki katika chaguzi mbalimbali za serikali.
Afisa uhamiaji
mfawidhi wa kituo cha uhamiaji Horohoro, Mrakibu Singwa Mokiwa alibainisha
kwamba wasafirishaji wakubwa wa wahamiaji haramu katika wilaya ya Mkinga ni
madereva Bodaboda ambao hutumia vipenyo ikiwemo eneo la kijiji cha Jasini hivyo
elimu hiyo imefika wakati muafaka ambapo itawasaidia madereva hao kutimiza
wajibu wao bila kuvunja sheria na kuilinda nchi yao dhidi ya wahamiaji haramu.
Mrakibu Mokiwa ametoa
wito kwa wananchi kwamba mlinzi namba moja wa mipaka ni mwananchi mwenyewe
hivyo wananchi wanatakiwa kuwa na uzalendo na nchi yao kwa kuwafichua wahamiaji
haramu ikiwemo kutoa taarifa kwa mamlaka husika.
Washiriki wa Mafunzo
hayo waliotoka katika makundi mbalimbali ya kijamii walikuwa na matarajio ya
kujua sheria za kuishi mipakani, kujua muhusika wa kwanza wa uhamiaji haramu,
jinsi ya kumtambua mhamiaji haramu na madhara ya kupitisha wahamiaji haramu
katika mipaka ya nchi yetu.
Yote hayo yalipatiwa ufumbuzi na wakufunzi Mrakibu Msaidizi wa Uhamiaji Azizi Kirondomara kutoka Kitengo cha Uhusiano Uhamiaji Makao Makuu, Bi Lucy Mseke Afisa Mradi Msaidizi IOM Tanzania na Bwana David Lukiri Kutoka Shirika la umoja wa mataifa la Wahamaji IOM.
HABARI PICHA NA MATUKIO
Yona Maki Mkuu wa Wilaya Mkinga |
Washiriki wa mafunzo ya Uhamiaji wakifuatilia kwa makini mafunzo yanayoendeshwa na IOM na Idara ya Uhamiaji katika kijiji cha Jasini Wilayani Mkinga Mkoani Tanga |
Afisa Uhamiaji Mfawidhi wa Kituo cha Uhamiaji Horohoro Mrakibu Singwa Mokiwa akiongea na washiriki wa mafunzo ya uhamiaji (Hawapo Pichani) katika kijiji cha Jasini kilichopo Wilayani Mkinga Mkoani Tanga mpakani mwa Tanzania na Kenya |
Baadhi ya washiriki waliohudhuria Mafunzo wakiwa katika Picha ya pamoja na Viongozi wa IOM na Idara ya Uhamiaji |
Mrakibu Msaidizi wa Uhamiaji Azizi Kirondomara kutoka Kitengo cha Uhusiano Uhamiaji Makao Makuu akiwasilisha moja ya mada ya madhara ya uhamiaji haramu nchini |
Lucy Mseke Afisa Mradi Msaidizi IOM Tanzania akieleza lengo la mafunzo |
David Lukiri Mmoja wa wakufunzi kutoka IOM akiwafundisha washiriki mbinu za kupambana na uhamiaji haramu katika maeneo ya mipakani |
Lucy Mseke kutoka IOM akifundisha moja ya mada za uhamiaji mpakani |
Washiriki wakifuatilia kwa makini mada zinzofundishwa |
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)