
Tukio hilo limeongozwa na aliyekuwa Msemaji Mkuu wa Idara ya Uhamiaji Mrakibu
Mwandamizi, Alhaj Ally Mohamed Mtanda ambaye amehamishiwa Wizara ya Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na kuongozwa na Mkuu wa kitengo cha
Habari ITV, Stephen Chuwa ambapo amekutana na kufanya mazungumzo na waandishi wa Habari wa ITV na Redio huku akiwahakikishia ushirikiano wa kutosha kama aliokuwa nao Msemaji Mkuu aliyepita.
Ikumbukwe kuwa Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Tanzania Dkt. Anna Peter Makakala amefanya mabadiliko madogo ya Uongozi kwa Wakuu wa Vitengo katika Makao Makuu ya Uhamiaji, Jijini Dodoma mapema wiki hii.
Katika Mabadiliko hayo, aliyekuwa Mkuu wa Kitengo cha Uraia, Mrakibu wa Uhamiaji, Paul John Mselle ameteuliwa kuwa Msemaji wa Idara ya Uhamiaji na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano.
Aidha, Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Makakala pia amemteua Mrakibu wa Uhamiaji Lucy Ansyline Nyaki kuwa Mkuu wa Kitengo cha Uraia. Kabla ya uteuzi huo, Nyaki alikuwa Afisa katika Kitengo cha Sheria Makao Makuu ya Uhamiaji.
Viongozi walioteuliwa katika nyadhifa hizo mpya wataanza kutekeleza rasmi majukumu yao kuanzia kesho tarehe 01 Aprili, 2020.
HABARI PICHA NA MATUKIO
![]() |
Msemaji Mpya wa Uhamiaji na Aliyepita wakiwa katika Moja ya redio za IPP Media, Kulia ni Mkuu wa kitengo cha Habari ITV, Stephen Chuwa |
Msemaji Mkuu wa Idara ya Uhamiaji Tanzania na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano Mrakibu wa Uhamiaji, Paul John Mselle (kulia) akibadilishana mawasiliano na waandishi wa Habari wa ITV |
Msemaji Mkuu wa Idara ya Uhamiaji Tanzania na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano Mrakibu wa Uhamiaji, Paul John Mselle (Kushoto) akiagana na Mkuu wa kitengo cha Habari ITV, Stephen Chuwa kwa salamu ya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa Corona kwa kutoshikana mikono |
Aliyekuwa Msemaji Mkuu wa Idara ya Uhamiaji Mrakibu Mwandamizi, Alhaj Ally Mohamed Mtanda akiagana na Mkuu wa kitengo cha Habari ITV, Stephen Chuwa kwa salamu ya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa Corona kwa kutoshikana mikono |
(Picha zote na Kitengo cha Uhusiano Uhamiaji Makao Makuu) |